Pages

Sunday, 8 February 2015

MALOBA



Sambusa ni chakula kinachopikwa kwa mchanganyiko wa viungo tofauti, vitu hivyo nikama vile nyama,vitunguu maji, napi unaweza kutia pilipil boga na kerot  kama utapenda. Vyakula kama sambusa maranying hutumiwa kwenye sehemu za sherehe au siku za skukuu.
Chapat  ni aina ya chakula kinachopikwa kwa kutumia  unga wa ngano, mafuta ya  kula, chumvi  na pia samli waweza kutia katika upishi huo. Mara nying chapti hupikwa kwa ajli ya chakula cha asubuhi ama usiku.
Maini  ni jamii ya kitoweo ambacho hupikwa kwa ajli ya kutowelea vyakula vyengine, kama chapatti na hata  maandaz. Pia chaweza kuliwa kama kiburudisho (kitafunwaji).

BIRIANI



Biriani ni chakula kinachoandaliwa kwa kutumia mchele pamoja na mchanganyiko wa vitu mbalimbali,
Kama vile mbatata, uzile, vitunguu maji na thom, mdalasini ,nyama au hata kuku, itategemea na wewe mwenyewe  kitoweo gani utapenda, na vyenginevyo.

VISHETI



Visheti  pia ni chakula ambacho hupikwa kwa kutumia unga wa ngano, sukari, hiliki na nazi iliyokunwa bila ya kuchujwa, hupikwa kwa kukanda unga, kukata na kuchoma kwa mafuta na baadae unatia sukari yako ambayo hujulikana kama ni shira. Mara nyingi visheti hivi huitwa vishet vya namba nane. Mara nyingi watu wa Zanzibar hula visheri hivi wakati wa asubuhi kwa chai.

MUHOGO



Muhogo ni jamii ya matunda ambacho wazanzibari wengi hukitumia kwa chakula, waweza kupika wa kuchemsha ama kwa kuuchanganya na nazi. Na pia ni futari kubwa ifikapo mwezi wa ramadhani. Pia muhogo hupikwa chipsi (chipsi za muhogo au makwaru).


TAMBI



Tambi, chakula hichi ni maarufu sana kwa wakaazi wa Zanzibar, na ni chakula maarufu katika mwezi mtukufu  wa ramadhani, tambi ni chakula kimoja ambacho hakisumbui katika kupika hupikwa kwakuchanganya sukari nanazi ama mafuta .

UROJO



Urojo ni chakula kinachopendwa sana na wakaazi wa zaznibar. Chakula hichi hupikwa kwa unga wa ngano, ndimu, bizari na chumvi na unapoliwa huchanganywa na badia, kachori, chipsi za muhogo, mishkaki na hata yai, urojo huliwa wakati wowote lakini mara nyingi huliwa asubuhi na usiku.