Pages

Sunday, 8 February 2015

NDIZI MBCHI NA MBIVU

Ndizi mbichi ni chakula kinachopendwa sana na wakaazi wa Zanzibar. Kuna aina mbali mbali za ndizi mbichi ndani ya visiwa vya zanzibar kama vile mtwike, koroboi,mzuzu, mkono wa mtembo na nyenginezo. Chakula hiki huweza kupikwa cha nazi au cha kuchemsha na kutowelewa na kitoweo kama vile samaki ama kachumbari na hata mboga. Lakini pia kuna ndizi mbivu ambazo nazo zinapendwa sana na wakaazi wa Zanzibar, nazo zinaweza kupikwa za nazi na kuliwa na hata kutowelewa kwa wali, zinapopikwa hutiwa hiliki na usukari kidogo ili kuongeza ladha nzuri

1 comment:

  1. Asante Bi mkubwa kwa kutuhabarisha kuhusu vyakula vyetu, Na nashkuru kwani nimefaidika na kufaidihsa pia. From Istanbul.

    ReplyDelete